Muda Unaisha: Ukweli Mchungu Ambao Watu Wengi Hawataki Kusikia
Niko macho. Niko makini. Na ninaelewa jambo moja ambalo watu wengi hawalitambui: muda unaisha. Na ukweli ni huu—unaisha pia kwako.
Muda Ndicho Kitu Pekee Usichoweza Kununua
Unaweza kupoteza shilingi milioni leo na ukazitengeneza kesho. Unaweza kufukuzwa kazi leo na ukapata nyingine kesho. Unaweza kupoteza kila kitu—isipokuwa muda.
Watu wanaofanikiwa wanaelewa hili kwa undani. Wanajua kuwa kila sekunde wanayoipoteza, hawatairudisha tena. Ndiyo maana wanaonekana kama wako mbioni kila wakati. Wanajenga. Wanaunda. Wanapambana.
Ushindi Hauko Kwenye Raha
Watu wengi hudhani mafanikio ni maisha mepesi, bila stress, bila matatizo. Huo ni uongo.
Ukweli ni huu:
- Asilimia 90 ya muda unahisi unapigwa na maisha
- Asilimia 8 unachanganyikiwa na unajiuliza kama ina maana
- Asilimia 2 tu ndipo unashinda na kuutumia vizuri
Washindi wa kweli hawapati amani kwenye ushindi—wanaipata kwenye mapambano.
Linda Muda Wako Kama Maisha Yako Yanavyoutegemea
Kwa sababu ukweli ni kwamba, maisha yako yanategemea muda wako.
Kama kila mtu anayekuzunguka anapoteza muda—anascroll simu masaa matatu, anaangalia TV masaa mawili, analala hadi saa sita mchana—na wewe ukasema “hapana”, basi tayari umejitenga na kundi.
Ukweli Watu Hawapendi Kukiri
Watu wengi hawana malengo. Hawana mwelekeo. Hawajui wanachotaka. Na kwa sababu muda wao hauna thamani, wanadhani muda wako pia hauna thamani.
Watataka ukae chini nao. Upoteze muda. Ucheke. Uchelewe. Lakini huwezi kuwa wa kawaida na wa kipekee kwa wakati mmoja.
Upweke Ni Bei ya Upekee
Njia ya mtu wa kipekee ni ya upweke. Hautalala kama wengine. Hutaparty kama wengine. Hutaspend muda kama wengine.
Na hilo ni sawa. Kwa sababu kama kila mtu angekuelewa, basi usingekuwa tofauti.
Miaka 5 Inaweza Kubadilisha Kila Kitu
Jiulize swali hili:
Sasa jiulize tena:
Jibu ni rahisi: chochote kinawezekana.
Hakuna Siri ya Mafanikio
Hakuna siri. Hakuna uchawi. Hakuna bahati.
Siri ni moja tu: Tumia muda wako vizuri kuliko mtu anayekufuata.
Amka mapema. Fanya kazi kwa bidii. Kataa visumbufu. Rudia kila siku.
Uamuzi Unafanywa Sasa
Huna jana. Ilishapita. Huna uhakika wa kesho. Ulichonacho ni sasa.
Na kila sekunde unayoishi, unachagua:
- Kuunda maisha unayotaka
- Au kupoteza maisha uliyopewa
Muda wako unaisha.
Usipoteze sekunde nyingine.
Anza leo. Anza sasa.
Choma boti zako. Linda muda wako. Shinda.
